Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaanzisha mpango wa kurejea nyumbani wakimbizi kutoka Angola

UNHCR yaanzisha mpango wa kurejea nyumbani wakimbizi kutoka Angola

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeanzisha mpango wa kuwarejesha nyumbani wakimbizi kutoka Angola walio kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Wakimbizi 252 wanarejeshwa nchini Angola kutoka mji wa Kimpese ulio kilomita 220 magharibi mwa Kinshasa. Shughuli za kurejea nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi kutoka DRC zilisimamishwa mwaka 2007 kufuatia ukosefu wa usafiri wakati huo. Kati ya mwaka 2003 na 2007 UNHCR ilisaidia wakimbizi 57,000 kurudi makwao kutoka nchini DRC. Alice Kariki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)