Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UNESCO umechagua wajumbe wapya 31 wa bodi ya wakurugenzi

Mkutano wa UNESCO umechagua wajumbe wapya 31 wa bodi ya wakurugenzi

Ujumbe unaohudhuria mkutano mkuu wa bodi ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, mjini Paris leo wamechagua wajumbe wapya 31 wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo.

Mkutano mkuu wa UNESCO unajumuisha nchi wanachama wa shirika hilo na una jukumu la kuunda sera na mpango wa kazi wa shirika hilo. Mkutano huo pia unachagua wajumbe wa bodi ya wakurugenzi 58 ambao washughulika na mfumo mzima wa utendaji wa shirika. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)