Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za chakula duniani zimeshuka kwa mwezi wa Oktoba:FAO

Bei za chakula duniani zimeshuka kwa mwezi wa Oktoba:FAO

Bei za chakula duniani zimeshuka zaidi mwezi wa Oktoba katika kipindi cha mizezi 11 imesema alhamisi ripoti ya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO. Hata hivyo FAO inasema bei za chakula bado ziko juu ukilinganisha na wakati kama huu mwaka jana.

Kwa mujibu wa shirika hilo bei za chakula zimekuwa wastani wa pointi 216 mwezi Oktoba zikiwa zimeshuka kwa asilimia 4 ikilinganisha na mwezi Septemba. Ripoti hiyo imetolewa kwa kuangalia bei za vyakula muhimu katika kiwango cha kimataifa, na hali hiyo imechangiwa na kushuka kimataifa kwa bei ya nafaka, mafuta ya kupikia, sukari na bidhaa zitokanazo na maziwa. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)