Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Familia za kifalme kuunga mkono msaada kwa watoto wanaokufa na njaa pembe ya Afrika

Familia za kifalme kuunga mkono msaada kwa watoto wanaokufa na njaa pembe ya Afrika

Familia za kifamle akiwemo Duke kutoka uingereza na mwana wa mfalme kutoka nchini Denmark wamekitembelea kituo cha shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ambapo wamezungumzia hali ya baadaye ya maelfu ya watoto ambao huenda wakafa njaa kwenye pembe ya Afrika ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.

Wakati wa ziara hiyo wote hao waliahidi kuunga mkono wito wa UNICEF wa msaada wa kusaidia mamilioni ya watoto walio kwenye hatari. Kwa sasa UNICEF inahitaji dola milioni 40 ili kuwahudumia watoto kwenye eneo hilo mwaka huu.