Katika mkutano wa G-20 Ban asisitiza mkataba mpya kwa karne ya 21

3 Novemba 2011

Tatizo la ukosefu wa ajira linaongezeka kila mahali, vijana wengi zaidi hawana kazi na wana matumaini madogo sana ya kupata ajira amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon siku ya Alhamisi akizungumza kwenye mkutano kuhusu kazi, unaofanyika mjini Cannes Ufaransa.

Katika mkutano huo unaofanyika sambamba na ule wa G-20 Ban amesema pengo la usawa wa kiuchumi linazidi kupanuka hivyo amesema mkutano huo wa G-20 ni lazima uwe zaidi ya kutafuta suluhu ya kiuchumi tu bali ni kuhusu ufufuaji wa kiuchumi wa kimataifa, ukuaji ambao ni endelevu na unaojumuisha wote.

Ameongeza kuwa lazima mkutano huo ulete mabadiliko ya kweli katika kufufua uchumi kwani wakati umewadia wa kuandika mkataba mpya kwa karne ya 21, na mkataba huo lazima ujumuishe suala la ajira kimataifa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud