Vijana wana nguvu ya kuweza kujenga vyema dunia:Migiro

2 Novemba 2011

Matukio yaliyojiri katika miezi kumi iliyopita duniani yanadhihirisha uwezo mkubwa walionao vijana katika kubadili dunia amesema naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro akiwataka vijana kusaidia kujenga maisha bora ya baadaye ya dunia hii.

Bi Migiro amesema dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi kuanzia tatizo la ajira, kutokuwepo kwa usawa hadi kuongezeka kwa hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema watu wana hamasi ya kujua mustakhbali wao leo na matarajio yao ya baadaye.

Bi Migiro ameyasema hayo katika chuo kikuu cha Missouri Kansas alipozungumza na wanafunzi na kusisitiza kwamba lazima kuwe na ajenda ya pamoja ambayo itasaidia kuhakikisha kwamba dunia ina amani, maendeleo, uhuru na haki kwa wote. Amesema wakati mwingine mchango wa vijana hauthaminiwi lakini lakini watu wanapaswa kuangalia yaliyojiri miezi kumi iliyopita na kutambua umuhimu wa vijana.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud