Mwenendo wa Mazingira unatisha maendeleo ya kimataifa kwa masikini:UNDP

2 Novemba 2011

Norway, Australia na Uholanzi zinashika nafasi ya juu duniani kwa mujibu wa ripoti ya maendeleo ya binadamu duniani mwaka 2011 iliyotolewa Jumatanio na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP. Lakini nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Niger na Burundi zinavuruta mkia katika ripoti hiyo ya kila mwaka inayopima maendeleo ya kitaifa katika masuala ya afya, elimu na kipato na kujumuisha nchi na serikali 187 duniani.

Nchi za Marekani, New Zeland, Canada, Ireland, Germany na Sweden zipo ndani ya kumi bora lakini linapokuja suala la kutokuwepo usawa katika masuala ya afya kitaifa baadhi ya mataifa tajiri yamejikuta yakitupwa nje ya 20 bora mfano Marekani imeporomoka kutoka nafasi ya 4 hadi ya 23, Jamhuri ya Korea kutoka namba 15 hadi 32 huku Israel ikianguka kutoka namba 17 hadi 25. Helen Clark ni mkurugenzi mkuu wa UNDP.

(SAUTI YA HELEN CLARK)

Mataifa 10 yanayoshika mkia yote ni kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, huku taifa lililoghubikwa na vita la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likishika nafasi ya mwisho kabisa. Mwandishi wa ripoti hiyo Jeni Klugman anaeleza pengo kubwa katika umri wa kuishi na fursa za kusoma kati ya walioshika nafasi za juu na wanaovuta mkia.

(SAUTI YA JENI KLUGMAN)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud