Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waonya kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu kwa watawa nchini China

UM waonya kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu kwa watawa nchini China

Kundi la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi uliopo kutokana na ripoti za ulinzi mkali uliowekwa ndani na nje ya kituo kinachowahifadhi watawa 2,500 kwenye eneo lililo kusini mashariki mwa China.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kidini Heiner Bielefeldt anasema kuwa dhuluma dhidi ya jamii ya watawa ni lazima ikome na ni lazima wapate haki yao ya kuabudu. Hii ni baada ya ripoti za kutumwa kwa vikosi vya usalama vikiwemo vya kupambana na ghasia na wanajeshi waliojihami kwenye barabara zinazoelekea kwenye makao ya watawa hao.