Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mengi yanasalia kufanyiwa WHO:Chan

Mengi yanasalia kufanyiwa WHO:Chan

Katibu Mkuu wa shirika la afya duniani WHO amesema kuwa mengi bado yanasalia kutekelezwa wakati wa hotuba yake kwa bodi kuu wa shirika hilo. Bi Chan amesema kuwa hali ya uchumi imekuwa mbaya suala ambalo limelilazimisha shirika hilo kuwa na mabadiliko akiongeza kuwa nchi zinahitaji huduma bora.

Amesema kuwa mabadiliko ndio mwanzo wa kupata matokeo mema wakati wajibu wao kama maafisa wa afya ukiwa ni kufanya kazi kwa njia inayostahili bila ya kupoteza wakati.