Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaendelea kusafirisha misaada kwenda nchini Uturuki

UNHCR yaendelea kusafirisha misaada kwenda nchini Uturuki

Ndege mbili zilizosheheni misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea nchini Uturuki zimewasili kwenye mji wa Erzurum zikiwa na mahema 1000 na mablanketi 20,000. Misaada hiyo itasafirishwa kwa magari kwenda sehemu zilizoathirika zaidi ukiwemo mji wa Ercis ulioshuhudia uharibifu mkubwa.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kwa sasa kunahitajika mahema 4000 , mablanketi 50,000 na matandiko 10,000 ya kulalia. Andrej Mahecic kutoka UNHCR anaeleza.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECICI)