Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasema kuwa wahamiaji kutoka Misri wanaorejea kutoka Libya wanahitaji misaada

IOM yasema kuwa wahamiaji kutoka Misri wanaorejea kutoka Libya wanahitaji misaada

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema kuwa wahamiaji raia wa Misri wanaorejea nyumbani kutoka nchini Libya kutokana na mzozo uliopo nchini humo wanahitaji msaada wa kuwawezesha kuanza upya maisha. Haya ni kutokana na utafiti uliofanywa na IOM kati ya wahamiaji 1,283 raia wa Misri walipokuwa wakihamishwa kutoka Tunisia na mji wa Misurata kwenda nchini Misri. Habari zaidi kuhusu mahitaji ya wahamiaji hawa pia zilipatikana kutoka kwa wizara ya uhamiaji nchini Misri. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)