Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wazorota kati ya mpaka wa Kenya na Somalia:OCHA

Usalama wazorota kati ya mpaka wa Kenya na Somalia:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa kuendelea kuzoroteka kwa usalama kati ya mpaka wa Kenya na Somalia kunatatiza utoaji wa misaada kwa maelfu ya waliothiriwa na ukame nchini Kenya na pia maelfu ya wakimbizi walio kwenye kambi ya Daadab.

Usalama pia unaripotiwa kuzorota kwenye miji ya Mandera na Wajir Kaskazini mwa Kenya. Kwenye kambi ya Daadab mashirika ya kutoa misaada yalisimamisha huduma zao baada ya kutekwa nyara kwa wafanyikazi wawili wa kutoa misaada tarehe 13 mwezi Oktoba. Kiasi kikubwa cha mvua inayonyesha kaskazini mwa Kenya pia imetatiza utoaji wa misaada, huku wafugaji wengine wakipoteza mifugo wao jinsi Elizabeth Brys anavyoeleza

(SAUTI YA ELIZABETH BRYS)