Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaomba misaada kusaidia watu nchini Korea Kaskazini

UNICEF yaomba misaada kusaidia watu nchini Korea Kaskazini

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kufadhili mpango wake wa kutoa lishe nchini Korea Kaskazini ambapo mamilioni ya wanawake wajawazito na watoto wanasumbuliwa na utapiamlo. Mwaka 2011 UNICEF ilitoa ombi la dola milioni 20.4 kwa huduma za dharura lakini hadi sasa imepokea dola milioni 4.6 tu. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)