Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka mashirikiano zaidi kuwashinda maharamia wa Somalia

UM wataka mashirikiano zaidi kuwashinda maharamia wa Somalia

Umoja wa Mataifa umetaka kuweko mashirikiano zaidi ili kushinda hujuma za kigaidi katika Pwani ya Somalia. Kulingana na mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa Tayé-Brook Zerihoun ni muhimu kwa jamii ya kimataifa kuongeza mashirikiano ya pamoja kuwakabili maharamia hao ambao wameendelea kuliweka katika hali tete eneo hilo.

Licha ya kusifu juhudi zinazoendelea kuchukulia ambazo baadhi zimezaa matunda kwa kukamwatwa maharaamia kadhaa, hata hivyo afisa huyo anataka ukurasa mpya wa mashirikiano ili kufanikisha shabaya ya kuwafagia kabisa.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji, kiasi cha watu 315 na vyombo vya usafiri 15 vinaendelea kushikiliwa na maharamia hao katika kipindi cha mwaka huu pekee.