Rais wa Baraza Kuu ataka usawa wa kimaendeleo

1 Novemba 2011

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amejadilia umuhimu wa kuhakikisha faida na fursa za kimaendelea zinatawanya kwa watu wote duniani hasa yale makundi ya watu maskini na akazitaka nchi zilizoaendelea kufikiria kuanzisha mbinu itayotumia kuratibu namna ya usambazwaji wa fursa hizo.

Kiongozi huyo amedokeza kile alichokiita nafasi ya maendeleo aendelevu akisema kuwa yanaweza kufikia kwa kuzingatia vigezo kama utayari, upatikanaji kwa wakati mahijati. Akihutubia mkutano wa kamati ya pili ya Umoja wa Mataifa Nassir ametaka kuwepo kwa shabaya ya pamoja ili kuzikabili changamoto za kimaendelea. Amezitaka pia jumuiya za kimataifa kuweka mafungamano ya pamoja ili hatimaye kufikia ukamilifu wa mambo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter