Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saif Al Islam huenda akajisalimisha ICC

Saif Al Islam huenda akajisalimisha ICC

Kuna taarifa kuwa huenda mtoto wa pili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Qadhafi, akajisalimisha kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Kwa mujibu wa mkuu wa mashtaka kwenye mahakama hiyo Luis Moreno Ocampo, mtoto huyo wa Qadhafi, Saif Al Islam Qadhafi, kumeanza kufanywa mawasiliano ambayo yanaashiri kuwepo kwa uwezekano wa kujisalimisha kwake.  Saif pamoja na aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa Abdullah Al-Senussi wametowekea mafichoni na inaaminika kuwa huenda watakuwa wamejichimbia huko Niger.

Duru za kimataifa zimesema kuwa zinaendeleza kampeni zake za kuwasaka watuhumiwa wote wawili.