Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauwaji ya waandamanaji Syria

Ban alaani mauwaji ya waandamanaji Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la kushambuliwa waandamanaji wa Syria iliyosababisha watu kadhaa kupoteza maisha na ameitaka serikali nchini humo kuzuia matumizi ya nguvu kudhibiti maandamano hayo.

Wananchi wa Syria wameendelea kujitokeza bara barani wakisisitiza haja ya kufanyika mageuzi ya kisiasa ili kufungua fursa zaidi za kidemokrasia. Ikiweka shabaya ya kuyaandama maandamano hayo, serikali ya Syria iliviamuru vikosi vyake kusambaratisha maandamano hayo na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha.

Ban ametaka mamlaka nchini humo kujizuia dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi akisema kuwa serikali inapaswa kusikiliza kilio cha wananchi.