Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yajiunga na UNESCO

Sudan Kusini yajiunga na UNESCO

Shirika la elimu , Sayansi , na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limelikaribisha taifa jipya la Sudan Kusini ambayo ndiyo nchi iliyo na viwango vya chini zaidi vya elimu duniani.

Kwenye sherehe zilizofanyika mjini Paris yaliyo makao makuu ya UNESCO bendera ya Sudan Kusini ilipandishwa kando na za wanachama wengine 193 wa UNESCO. Sherehe hiyo iliandaliwa siku mbili baada ya Sudan Kusini kukamilisha kutimiza mahitaji ya katiba ya shirika hilo.

Kwenye sherehe hizo mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema kuwa taifa la Sudan Kusini linakabiliwa na changamoto nyingi lakini akaahidi kuwa Shirika lake litaisadia Sudan Kusini kujenga mifumo ya elimu na pia kuwapa mafunzo waalimu