Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu mpya wa mipango ya Usalama wa UM azuru Darfur

Mkuu mpya wa mipango ya Usalama wa UM azuru Darfur

Mkuu mpya wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa amezuru kwa mara ya kwanza kituo kimoja kati ya 16 vya operesheni za Umoja wa Mataifa duniani. Herve Ladsou amechagua kituo kikubwa cha operesheni ambacho ni Darfur Sudan na amekutana na maafisa wa serikali wa eneo hilo, jumuiya za kijamii na wafanyakazi wa mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika Darfur UNAMID.

Bwana Ladsou na mkuu wa UNAMID Ibrahim Gambari wametembelea mji wa kaskazini mwa jimbo hilo wa Shangil Tobaya kukutana na jumuiya ya viongozi ambapo wamejadili masuala ya maendeleo hususani suala la elimu na upatikanaji wa maji. Bwana Ladsou amesisitiza kwamba mchakato wa amani lazima uongozwe na Wadarfur wenyewe na kwamba juhudi za Umoja wa Mataifa zina lengo la kuhakikisha mchakato huo unajumuiya pande zote.