Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirika katika kilimo ni muhimu kwa kupunguza umaskini na njaa:FAO, IFAD WFP

Ushirika katika kilimo ni muhimu kwa kupunguza umaskini na njaa:FAO, IFAD WFP

Wakulima wadogowadogo wanafaidika sana kwa ushirika wa kilimo ikiwemo uwezo wa kushawishi masuala ya bei na kushirikiana rasilimali ambazo zinasaidia kupunguza umasikini na kuleta usalama wa chakula kwa mamilioni ya watu limesema shirika la chakula na kilimo FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Tamko hilo limetolewa katika hafla maalumu ya uzinduzi wa mwaka wa kimataifa wa ushirika 2012 yaani IYC mjini New York. Mashirika hayo yamesema umuhimu wa ushirika wa kilimo na kuimarisha maisha ya mamilioni ya wakulima wadogowadogo na familia zao usipewe kisogo.George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)