Nchini Somalia hali bado ni tete lakini matumaini ya amani bado yapo:Mahiga

31 Oktoba 2011

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema hali ya usalama nchini Somalia bado ni tete lakini kuna matumaini kuwa punde mambo yataanza kuwa shwari.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi Kenya hii leo balozi Mahiga amesema maeneo yanayoshikiliwa na wanamgambo wa Al-Shabaab bado kuna hofu sana, watu wanaendelea kukimbia na mashirika ya misaada yanashindwa kuwafikia watu wanaohitaji msaada kutokana na usalama mdogo. Ameongeza kuwa ana imani kuwa operesheni ya pamoja inayoendeshwa na jeshi la serikali ya mpito ya Somalia na majeshi ya serikali ya Kenya dhidi ya wanamgambo hao ikikamilika itarejesha hali ya utulivu Somalia.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter