Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Haki za Binadamu akaribisha mwanahaki wa bilioni 7

Mkuu wa Haki za Binadamu akaribisha mwanahaki wa bilioni 7

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay leo amekaribisha mtoto aliyezaliwa na kuifanya idadi ya watu duniani kufikia bilioni saba kwa ahadi ya kuzingatia azimio la kimataifa la haki za binadamu. Amesema kisheria mtoto huyo awe wa kike au wa kiume amezaliwa huru na usawa katika utu na haki za binadamu.

Ameongeza kuwa tangu mtoto huyo akizaliwa kama alivyomtoto mwingine leo au siku nyingine yoyote ni lazima ahahakikishiwe uhuru, bila hofu , kulindwa kutokana na ubaguzi, ukatili na fursa sawa ya usalama, haki na kuheshimiwa kama mwanachama mpya wa familia ya dunia. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)