Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumzia ghasia kati ya Israel na Ukanda wa Gaza

Ban azungumzia ghasia kati ya Israel na Ukanda wa Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa hisia zake kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa kusini mwa Israel na kwenye ukanda wa Gaza ambapo watu kadha wameuawa. Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amelaani shambulizi la roketi lililoendeshwa kutoka ukanda wa Gaza ambalo lilisabaisha kifo cha raia mmoja wa Israel.

Ban pia ameitaka Israel kujizuia katika kuchukua hatua baada ya wanajeshi wa Isreal kuripotiwa kuwaua wanamgambo 10 kwenye ukanda wa Gaza. Ban ameongeza kuwa ofisi ya mratibu wa masuala ya amani eneo la mashariki ya kati Robert Serry inafanya kila jitihada katika kumaliza mzozo huo.