Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuondosha ziada ya risasi kwenye nishati ya mafuta kutanufaisha afya za wengi-Utafiti

Kuondosha ziada ya risasi kwenye nishati ya mafuta kutanufaisha afya za wengi-Utafiti

Utafiti mmoja unaonyesha kuwa iwapo kutowekwa zingatia la kuondoa ziada ya risasi inayowekwa kwenye nishati ya mafuta, ulimwengu unaweza kupiga hatua kubwa na kufanikiwa kuzikwepa gharama zizozo za lazima.

 Kwa mujibu wa utafiti huo unaungwa mkono na Umoja wa Mataifa,matokeo kadhaa yamejidhihirisha ikiwemo kupunguza gharama za uzalishaji, kuokoa vifo visivyo vya wakati vinavyojiri sasa pamoja na kuwepo uwezekano wa kupungua kiwango cha uhalifu.

 Baadhi ya nchi tayari zimeanza kutekeleza shabaya hiyo ya uondoaji wa ziada kwenye nishati ya mafuta. Nchini Marekani ambako mpango huo umeanza kutekelezwa kunaripotiwa kupatikana kwa mafanikio.

 Nishati ya mafuta ambayo hukolezwa kemikali aiana ya risasa inatajwa kuleta madhara makubwa ikiwemo uharibifu wa mazingira na kusababisha matatizo ya kiafya kwa baadhi ya watu.