Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila watu saba, watano kati yao hawana uhakika wa ustawi wa kijamii

Kila watu saba, watano kati yao hawana uhakika wa ustawi wa kijamii

Kundi la wataalamu wa mambo limetoa mwito likizitaka serikali duniani kuongeza mafungu ya kipato na kuboresha hali ya ustawi wa kijamii ili hatimaye kufadhilia amani na usalama pamoja na ukuzaji uchumi.

Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO, zaidi ya watu bilioni 5 duniani kote hawana uhakika wa ustawi wa kijamii. Wakati huo huo zaidi ya asilimia 15 ya wakazi wa dunia ambao hawana ajira hupata malipo kama vile wameajiriwa.

Kwa lugha nyingine ni kusema kuwa kila penye watu saba basi watano kati yao hawana istahiki ya kijamii.