Mamia ya wakimbizi kutoka Sudan walikimbia eneo la Blue Nile na kuingia Ethiopia

28 Oktoba 2011

Mashambulizi ya anga kwenye jimbo la Blue Nile nchini Sudan yamewalazimu wakimbizi zaidi kuhama eneo hilo na kukimbilia Ethiopia. Kwa muda wa siku nne zilizopita karibu wakimbizi 2000 kutoka Sudan wamewasili magharibi wa Ethiopia huku Wengi wakiwa ni wanawake, watoto na watu wazee.

Ripoti zinasema kuwa wapiganaji waliojihami kutoka upande wa Sudan wanajiandaa kulipiza kisasi. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud