Theluji na mvua yaikumba uturuki ambako waliokufa na tetemeko wamefikia 532

27 Oktoba 2011

Theluji na mvua vinatatiza shughuli za uokozi kufuatia tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki huku idadi ya waliokufa ikizidi 500 umesema uongozi wa nchi hiyo. Tetemeko lililikumba eneo la Mashariki la Van Jumapili iliyopita na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Umoja wa mataifa umepongeza juhudi za haraka za serikali kukabiliana na janga hilo kwa kutuma waokozi 4000. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA Elisabeth Byrs anasema kipaumbele hivi sasa ni kuhakikisha walionusurika wanasaidiwa na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepeleka mahema 4000 kwa chama cha msalaba mwekundu cha Uturuki.

Nalo shirika la idadi ya watu duniani UNFPA litatioa mahema 200 ya kujikinga na baridi kwani joto linashuka chini ya nyuzi sufuri wakati wa usiku na litafuatilia kwa karibu hali ya afya ya waathirika hao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud