Israel na Palestina waafiki kutoa mapendekezo ya amani:UM

27 Oktoba 2011

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kidiplomasia katika kutafuta amani ya Mashariki ya Kati wamekutana katika nyakati tofauti na maafisa wa Israel na Palestina mjini Jerusalem, na pande zote kuafiki kutoa mapendekezo ya kina ya utaifa na usalama ndani ya miezi mitatu.

Jopo hilo lijulikanalo kama Quartet linalojumuisha Umoja wa Mataifa, muungano wa Ulaya, Urusi na Marekani lilikuwa linafatilia mikakati waliyoizindua mwezi uliopita ya kuzikutanisha Israel na Palestina tena kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo ya amani mwaka jana. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter