Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliberia wametakiwa kuendesha duru ya pili ya uchaguzi kwa amani na utulivu

Waliberia wametakiwa kuendesha duru ya pili ya uchaguzi kwa amani na utulivu

Baraza la Usalama limewataka Waliberia kuendesha duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Novemba 8 kwa amani na usalama. Matokeo ya awamu ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 11 na kutangazwa Jumanne ya wiki hii yameonyesha kwamba rais aliyeko madarakani Ellen Johnson-Sirlef anaongoza kwa asilimia 43.9 ya kura zote akifuatiwa na bwana Tubman aliye na asilimi 32.7.

Wagombea hao wawili wanaongoza kwa kura watachuana tena katika awamu ya pili. Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Oktober balozi Joy Ogwu wa Nigeria amesema wajumbe wa baraza wanawachagiza Waliberia kushirikiana kujenga imani ya mfumo wao wa uchaguzi.

(SAUTI YA JOY OGWU)