Zaidi ya dola bilioni moja kwa waathirika wa uvamizi wa Iraq nchini Kuwait:UM

27 Oktoba 2011

Zaidi ya dola bilioni moja zimetolewa na tume ya fidia ya Umoja wa Mataifa UNCC hii leo kwa ajili ya kulipa fidia madai manane ya walioathirika na kupoteza kila kitu wakati Iraq ilipoivamia Kuwait mwaka 1990.

Malipo ya leo ya dola bilioni 1.3 yanafanya jumla ya fidia iliyolipwa na tume hiyo hadi sasa kufikia dola bilioni 34.3 zilizolipwa kwa serikali na mashirika ya kimataifa zaidi ya 100 na maashi, fedha ambazo zimegawanywa kwa madai milioni 1.5. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter