Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa chakula ni muhimu:Ban

Usalama wa chakula ni muhimu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema siku ya chakula duniani mwaka huu imeadhimishwa wakati ambapo Pembe ya Afrika inakabiliwa na ukame mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 60. Amesema na sehemu zilizoathirika zaidi ni zile za Kusini mwa Somalia ambazo ni vigumu wafanyakazi wa misaada kuzifikia.

Kwengineko amesema hali bado ni mbaya na mifgo, chakula na mbegu zimeharibika vibaya na huenda hatari ya hali hiyo ikaendelea. Akizungumza katika hafla maalumu ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya chakula duniani ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba Ban amesema janga la sasa Pembe ya Afrika ni kubwa na tofauti nay ale yaliyotokea siku za nyuma kwenye ukanda huo.

Amesema hata hivyo serikali zilizoathirika kwa msaada wa wadau wengine wa maendeleo wamejitahidi kupambana na janga hilo, juhudi zao zimeokoa maisha ya mamilioni ya watu na kuzisaidia jamii kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Ameongeza kuwa janga hilo limedhihirisha wazi kwamba hatua madhubuti zikichukuliwa basi zitahakikisha kuna usalama wa chakula.