Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaweka lugha ya kichina kwenye mtandao

WFP yaweka lugha ya kichina kwenye mtandao

Shirika la kimataifa linalohusika na mpango wa chakula WFP, limeongeza gia kwenye harakati zake za kukabiliana na tatizo la njaa dunia kwa kuanzisha mpango wa lugha ndani ya mtandao. Watumiaji wa mtandao huo sasa wataweza kujifunza lugha na maneno mapya ambayo yamefungamanishwa katika lugha ya kichina.

Waratibu wa mpango huo wamesema kuwa sasa raia wa China watapata fursa ya kujifunza maneno mapya ya kingereza na hivyo kuongeza uwanja wa mawasiliano.