Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azipongeza taasisi zisizo za kiserikali

Ban azipongeza taasisi zisizo za kiserikali

 

Uwepo wa taasisi zisizo za kiserikali ni muhimu hasa wakati huu ambapo dunia inalenga shabaya ya kufikia amani na usalama. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye alikuwa akizungumza kwenye kongamano moja lililoyaleta pamoja mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali.

Ban amepongeza mchango mkubwa kutoka kwa taasisi hizi zisizo za kiserikali ambazo amesema kuwa zimeweka zingatio kubwa kwenye uimarishaji ustawi wa jamii. Amesema taasisi hizi ni muitifaki mkubwa wa Umoja wa Mataifa na amehaidi kuendelea kutambua mchango wao.