27 Oktoba 2011
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ameelezea umuhimu uliopo kwenye ushirikiano wa kimataifa katika kukabilina na hali mbaya ya uchumi duniani.
Akiongea alipoongoza mkutano kwenye makao makuu ya UM wa kujadili mkutano wa mataifa tajiri na yanayoinukia kiuchumi ya G20 utakaondaliwa wiki ijayo Al-Nasser amesema kuwa masuala mmakuu kama haya sio ya nchi moja tu akiongeza kinachoathiri nchi moja kinaathiri nchi zote. Ameongeza kuwa kukabilina na uchumi mbaya duniani ni sula litafanikiwa tu iwapo kutakuwa na ushirikiano wa karibu na mazungumzo yaliyo wazi.