Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Thamani ya urithi wa matukio ya sauti, video na picha ni kubwa kwa dunia:UNESCO

Thamani ya urithi wa matukio ya sauti, video na picha ni kubwa kwa dunia:UNESCO

Umoja wa Mataifa leo umetanabaisha umuhimu wa kuhifadhi urithi wa dunia katika sauti, video na picha, ukisisitiza hatari ya kuharibika matukio yaliyorekodiwa kwa njia ya sauti, filamu au video, na kusema kuna haja ya juhudi za kuhakikisha kwamba zinahifadhiwa vizuri kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Likiadhimisha siku ya kimataifa ya urithi wa sauti na filamu au video ambayo kauli mbiu yake mwaka huu ni “sikia, ona na jifunze” shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO limesema matukio muhimu yaliyorekodiwa yametoweka tangu kuzinduliwa kwa teknolojia ya picha na sauti. UNESCO imeongeza kuwa kwa kutoweka huko dunia imepoteza njia ya kushirikiana na wengine uzoefu, ubunifu na ujuzi. Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova akitoa ujumbe maalumu kuhusu siku hii amesema

(SAUTI YA IRINA BOKOVA)

Ameongeza kuwa ili kulinda urithi wa sauti, picha na filamu au video hatua madhubuti lazima zichukuliwe, mafunzo yatolewe na msaada wa kitaalamu unahitajika kwa wafanyakazi wa makumbusho, maktaba na taasisi husika. Umoja wa Mataifa unamiliki maktaba mjini New York iliyo na saa 80,000 sauti zilizorekodia, tapu 70,000, saa 37,700 za filamu, video 25,000 na picha zaidi ya 800,000 na kila siku zinaongezwa mpya.