Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kutoa usadizi zaidi kwa nchi zinazofanya uchaguzi

UM kutoa usadizi zaidi kwa nchi zinazofanya uchaguzi

Mkurugenzi wa masuala ya kisiasa kwenye Umoja wa Mataifa Lynn Pascoe amesema kuwa Umoja wa Mataifa utahitaji kutoa usaidizi zaidi kando na usaidizi wa kiufundi kwenye uchaguzi kwa kuwa changuzi nyingi huwa zinafautiwa na ghasia.

Akihutubia wajumbe kwenye kamati inayohusika na masuala ya kijamii na kibinadamu Pascoe amesema kuwa mara nyingi uchaguzi ndio unakuwa mwanzo wa ghasia kwa hivyo Umoja wa Mataifa unahitaji kuhakikisha kuwa wanachama wake wamepewa usaidizi unaohitajika.

UM umesaidia zaidi ya nchi 50 kwa muda wa miaka miwili iliyopita zikiwemo Afghanistan na Zimbabwe huku ukiendelea kupokea maombi zaidi.