Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zakubaliana kupiga marafuku masalia ya bidhaa zenye kuleta sumu

Nchi zakubaliana kupiga marafuku masalia ya bidhaa zenye kuleta sumu

Kuna uwezekano wa kuanza kutumika kwa azimio la pamoja linalotaka kuzuia usafirishaji wa masalia ya vitu ambavyo ni hatari kutoka katika nchi zilizoendelea kupelekwa katika nchi zinazoendelea.

Makubaliano hayo ambayo yanajulikana kama "Ban Amendment" yanaweza zingatio la uzuiaji usafirishaji wa bidhaa zozote zilizokwisha tumika ambazo zinaweza kuleta madhara pale zinaposafirishwa hadi katika nchi za dunia ya tatu.

Matumaini ya kuanza kutumika kwa mkataba huo yalijitokeza huko Cartagena, Columbia baada ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP kufanikiwa kuzileta pamoja nchi kadhaa na kufikia makubaliano. Kulingana na shirika hilo la Umoja wa Mataifa nchi nyingine 17 zimeridhia mkataba huo ambao ulianza kujadiliwa tangu miaka 15 iliyopita.