Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi wajumuishwe kwenye mchakato wa amani Darfur:UM

Waasi wajumuishwe kwenye mchakato wa amani Darfur:UM

Wakati hatua muhimu zimepigwa katika mchakato wa amani kwenye jimbo la Darfur Sudan, juhudi zaidi zinahitajika ili kuwajumuisha waasi kwenye mchakato huo ambao bado wanapambana na majeshi ya serikali amesema mkuu wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Herve Ladsou ameliambia Baraza la Usalama kwamba anazitaka pande zote ambazo hazijasitisha vita kufanya hivyo na kujiunga kwenye majadiliano ya amani mara moja na bila masharti yoyote, akikumbusha mkataba wa amani wa Doha uliotiwa saini kati ya serikali ya Sudan na moja ya makundi ya waasi la Liberation and Justice Movement LJM.

Bwana Ladsou aliwasilisha ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuhusu mpango wa amani wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na mungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur UNAMID.