Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM Libya amesema ukombozi wa Libya ni ukurasa mpya

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM Libya amesema ukombozi wa Libya ni ukurasa mpya

 

Mratibu wa masauala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya George Charpentier amezuru mji wa Sirte Libya leo akifungua njia ya mpango wa tathimini ya mji huo na Ban walidi utakaohitimishwa siku mbili zijazo.

Mpango huo unafuatia zoezi la kuandaa usambazaji wa misaada ya kibinadamu karibu na maeneo hayo katika maandalizi ya kumaliza vita. Msaada huo wa kibinadamu ni pamoja na chakula, vifaa visivyo chakula na maji. Bwana Charpentier amesema mbali ya msaada ho mambo mengine wanayoyapa kipaumbele ni kurejesha huduma ya umeme, maji,kusafisha mabaki yote ya silaha na mabomu na makazi kwa ajili ya raia watakaokuwa wakirejea nyumbani.

(SAUTI YA GEORG CHARPENTIER)