Ripoti ya pamoja ya UNCTAD, OECD na WTO yasema kuna haja ya G20 kuchukua hatua haraka

26 Oktoba 2011

Ripoti ya pamoja ya shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo na biashara UNCTAD, shirika la kimataifa la biashara WTO na shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD imebaini kwamba uchipukaji wa uchumi baada ya mdororo unakabiliwa na changamoto mpya na huenda ukuaji wa uchumi katika nusu ya pili ya mwaka 2011 ukapungua.

Kufuatia hali hiyo mashirika hayo yamezitolea wito nchi za G-20 kuchukua hatua zaidi za haraka na kuendelea kutimiza ahadi zake. Hata hivyo ripoti hiyo imeongeza kuwa kuna mafanikio kiasi yanayoonekana kutokana na hatua zinazochukuliwa na mataifa hayo kama kuelekea kukomesha kabisa vikwazo katika uwekezaji toka nje na kuboresha mazingira ya uwekezaji. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud