Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati watu kufikia bilioni 7, juhudi zahitajika za maendeleo kwa wote:UNFPA

Wakati watu kufikia bilioni 7, juhudi zahitajika za maendeleo kwa wote:UNFPA

 

Katika siku tano zijazo idadi ya watu duniani inatazamiwa kufikia bilioni 7, na jinsi hatua zitakavyochukuliwa sasa itatanabaisha endapo kuna mstakhabali mzuri wa afya, endelevu na wa matuamaini ya baadaye au mustakhabali tuakaoghubikwa na kutokuwepo sawa, uharibifu wa mazingira na matatizo ya kiuchumi.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya hali ya idadi ya watu kwa mwaka 2011 iliyochapishwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA. Mkurugenzi mkuu wa UNFPA Dr Babatunde Osotimehin amesema kukiwa na mipango na uwekezaji muafaka kwa watu hivi sasa, katika kuwawezesha kufanya maamuzi ambayo sio tuu kwa faida yao bali kwa faida ya dunia nzima. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)