Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali inazidi kuwa mbaya nchini Uturuki

Hali inazidi kuwa mbaya nchini Uturuki

Hali inaripotiwa kuendelea kuwa mbaya nchini Uturuki baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi . Maelfu ya watu bado wanakisiwa kukwama nchini ya vifusi huku bado ikiwa haijatolewa idadi ya watu ambao bado hawajulikani walipo.

Inakadiriwa kuwa majengo 2,256 yameharibiwa wakati wa janga hilo. Shughuli kuu kwa sasa ni kusambaza mablanketi, chakula na vifaa vya kupasha joto wakati viwango vya baridi vikiwa ni vya chini. Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa bado maelfu ya watu wamefunikwa kwenye vifusi kwenye tetemeko lililosababisha vifo vya karibu watu 366 mashariki mwa Uturuki na wengine 1300 kujeruhiwa. Jesicca Sallabank ni msemaji wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.

(SAUTI YA JESICCA SALLABANK)

Wakati huo huo rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ameonyesha huruma kwa serikali na wananchi wa Uturuki kutokana na maafa na uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo.