Mvua yasababisha madhara nchini El Salvador, Guatemala, Honduras na Nicaragua

25 Oktoba 2011

Mataifa ya El Salvador, Guatemala, Honduras na Nicaragua yako kwenye hali ya tahadhari kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo tangu tarehe 12 mwezi huu ambapo zaidi ya watu milioni 1.2 wameathirika. Elisabeth Byrs kutoka ofisi la kuratibu masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa anasema kuwa ombi mpya la dola milioni 15.7 litatolewa nchini El Salvador fedha ambazo zitawasaidia watu 300,000 kwa muda wa majuma sita yajayo.

Zaidi ya watu 56,000 wamelazimika kuhama makwao nchini El Salvado huku asilimia 69 ya taifa hilo ikiathiriwa na mvua hiyo. Hali ya afya pia inatajwa kudorora huku kukiripotiwa magonjwa yanayosababishwa na mafuriko.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud