Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuchunguza kunyongwa kwa watu 53 nchini Libya

UM kuchunguza kunyongwa kwa watu 53 nchini Libya

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanyika uchunguzi kwenye ripoti inayoeleza kunyongwa kwa watu 53 kwenye mji wa Sirte nchini Libya. Shirika la Human Rights Watch linasema kuwa lilishuhudia maiti za wafuasi wa aliyekuwa rais wa Libya Muammar Gaddafi ambao mikono ilikuwa imegungwa na kuachwa kwenye hoteli moja mjini Sirte.

Msemaji wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Ravina Shamsadani anasema kuwa Umoja wa Mataifa umesoma ripoti kuhusu mauaji hayo na kuwa itafanya uchunguzi. Aditya Mehta wa Radio ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Shamsadani kuhusu umuhimu wa kumaliza ukwepaji wa sheria ndani mwa Libya mpya.

(SAUTI YA RAVINA SHAMSADANI)