Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana kutoa maoni kuhusu ugonjwa wa ukimwi

Vijana kutoa maoni kuhusu ugonjwa wa ukimwi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la UNAIDS linazindua mradi kwenye mtandao unaowalenga vijana na ugonjwa wa ukimwi. Mradi huo unatumiwa kuwawezesha idadi kubwa ya watu kuweka mikakati, kutatua matatizo au kutoa maoni mapya.

Wakati ambapo vijana 3000 walio kati ya miaka 15-24 wakiambukizwa na ugonjwa wa ukimwi kila siku suala la kubuni njia mpya za mawasiliano za kubadilishana maoni kwenye mtandao ni bora katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi. Watu walio kati ya miaka 15-29 wanaruhusiwa kushiriki kwenye mradi huo ambao utadumu kwa muda wa miezi miwili hadi mwezi Januari mwaka 2012.