Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa heshima kwa jaji Antonio Cassese

Ban atoa heshima kwa jaji Antonio Cassese

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa heshima zake kwa jaji Antonio Cassese ambaye ni mtaalamu maarufu wa sheria aliyeaga dunia ijumaa iliyopita akimtaja kama bingwa wa sheria ya kimataifa na rafiki wa Umoja wa Mataifa. Jaji Cassese ambaye amekuwa mwalimu wa sheria kwa miaka mingi sehemu mbali mbali za dunia aliaga dunia akiwa nyumbani kwake kwenye mji wa Florence nchini Italia akiwa na umri wa miaka 74. Jaji Cassese aliusaidia Umoja wa Mataifa kwenye masuala mengi.

Pia alihudumu kama rais wa kwanza wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu Yugoslavia ya Zamani na rais wa kwanza wa mahakama ya kimataifa kuhusu Lebanon.