Ban awapongeza watunisia kwa kufanya uchaguzi kwa mpango na amani

24 Oktoba 2011

Watunisia na serikali ya mpito ya nchi hiyo wamepongezwa kwa kuendesha uchaguzi wa kihitoria wa bunge Jumapili ya October 23. Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema huu ni uchaguzi muhimu na hatua kubwa kuelekea demokrasia ya Tunisia, na ni maendeleo katika mabadiliko ya kidemokrasia Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Ban amewachagiza wadau wote nchini humo kutimiza ahadi zao za kujumuisha wote na kuwa na wazi katika sehemu ya pili iliyosalia ya mchakato wa kipindi cha mpito. Ameongeza kuwa ushiriki wa wanawake na vijana katika mabadiliko ni kitovu cha mafanikio. Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanatarajiwa Jumanne wiki hii.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter