UM kuendelea kusaidia Libya wakati viongozi wapya wakitangaza ukombozi

24 Oktoba 2011

Umoja wa Mataifa umerejea kusisitiza nia yake ya kuwasaidia watu wa Libya kujenga mustakhbali mzuri wa taifa lao wakati viongozi wa baraza la mpito NTC walitangaza ukombozi kamili wa taifa hilo la Afrika ya Kaskazini ikiwa ni miezi minane tangu kuanza kwa vuguvugu na machafuko.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema tangazo la ukombozi lililotolewa siku ya Jumapili mjini Benghazi na NTC linaweka historia ya watu kufikia lengo la kuwa na uhuru baada ya miongo zaidi ya minne ya udikteta. Amesema sasa Libya ndio itakayoshika hatma yao ya serikali yao ambayo kwa mjibu wa NTC itakuwa ya haki na mardhiano ya kitaifa.

Tangazo la NTC la ukombozi limetolewa siku tatu baada ya kifo cha aliyekwa rais wa nchi hiyo kwa miaka 42 Kanali Muammar Gaddafi aliyeuawa Alhamisi iliyopita mjini Sirte ambapo pia mwanae mmoja wa kime aliawa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud