Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM uko tayari kusaidia waathirika wa tetemeko Uturuki

UM uko tayari kusaidia waathirika wa tetemeko Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amestushwa na kuhuzunishwa na athari za tetemeko la ardhi lililotokea Jumapili nchini Uturuki na kupoteza maisha ya watu, kujeruhi wengine na kuharibu miundombinu. Ban amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada kama utaambwa kufanya hivyo.

Watu zaidi ya 200 wamearifiwa kufa na 1,300 kujeruhiwa wakati tetemeko la ukubwa wa 7.2 vipimo vya rishta lililolikumbwa eneo la karibu na mji wa Van. Watu wengine wengi inasemekana bado wamenasa kwenye vifusi. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)