Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania inajiandaa kwa kufanya sensa ya kitaifa:UNFPA

Tanzania inajiandaa kwa kufanya sensa ya kitaifa:UNFPA

Idadi ya watu nchini Tanzania inakuwa kwa kiwango cha asilimia 2.9 ikiwa ni wastani wa watu milioni 1.3 kila mwaka kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA. Mwaka 2012 taifa hilo la Afrika ya Mashariki limepanga kuendesha sensa ya kitaifa ambayo inakadiriwa kugharimu dola milioni 76.

Kama sehemu ya maandalizi sensa ya majaribio inafanyika hivi sasa kwa wiki nzima katika baadhi ya mikoa na wilaya za nchi hiyo. UNFPA imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na serikali ya Tanzania kuhakikisha zoezi hilo linaendelea vizuri. Mwakilishi wa UNFPA Tanzania ni Dr Julitta Onabanjo.

(SAUTI YA JULITTA ONABANJO)